Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Waziri Waziri Kindamba amewahimiza wakulima mkoani Songwe kujikita katika kilimo cha mazao ya muda mfupi ili kuendana na utabiri uliofanywa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuwa mwaka huu kutakuwa na mvua chache za vuli zitakazonyesha kwa muda mfupi.
Mhe. Kindamba ametoa wito huo kwa watalaamu wa Halmashauri kwenda kutoa elimu na hamasa kwa wakulima kujiandaa na kilimo cha muda mfupi kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
"Kuna uwezekano mkubwa mvua zinaweza kuwa chache hasa halmashauri zinazotegemea kilimo sana, kama Momba na Songwe nendeni mkaongee na wananchi wenu ili waweze kujipanga vizuri na pia kuzalisha mazao ya muda mfupi"
Mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa mkoa wa Songwe unategemewa na mikoa mingi na mataifa jirani kwa kuzalisha mazao, njia pekee ya kuendelea kutegemewa ni kuzalisha mazao mengi ambayo yatafanya mkulima apate na akiba ya kuuza.
Katika hatua nyingine, Mhe. Kindamba amezitaka Halmashauri kasimamieni zoezi la ugawaji wa mbolea ya ruzuku kwa wakulima kwani kuna baadhi ya wafanyabishara wamegeuza mbolea hizo kuwa fursa ya kujipatia fedha za udanganyifu.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.