Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa Songwe [ALAT] imeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Songwe kwa kusimamia vyema ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Songwe ambao umeifanya kuwa na majengo ya kisasa.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Songwe Mhe. Ubatizo Songa Leo Jumanne Mei 2, 2023 mara baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Hospitali hiyo ambapo amesema ujenzi huo umesimamiwa vizuri ndiyo maana majengo ni bora na ya kisasa.
Mhe. Songa ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje na Diwani wa Kata ya Bupigu amesema muonekano wa majengo kwa nje hata ndani unaendana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Nimetazama haya majengo kwa kweli yanapendeza sana. Natamani kuona majengo kama haya yakijengwa kwenye maeneo mengine ya mkoa wetu", alisema Mhe. Songa.
Mhe. Mathew Chikoti, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba mbali na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Songwe kwa ujenzi wa Hospitali hiyo zaidi ameipongeza kwa kuanza kutoa huduma za afya ambapo mpango huo ameuelezea kuwa unapunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu mkoani Mbeya.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe CPA. Cecilia Kavishe akiwasilisha taarifa ya ujenzi huo mbele ya Wajumbe wa ALAT Mkoa amesema mpaka sasa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Songwe umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.6 ukihusisha majengo mbalimbali kama OPD, EMD, Wodi 3, jengo la Mama na Mtoto, na jengo la Uzazi
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.