Katika kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Songwe wanapata huduma ya usafiri na usafirishaji nyakati zote, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga kiasi cha shilingi bilioni 2.07 kwa Tarura kwa ajili ya kujenga na kuboresha barabara kupitia bajeti ya fedha mwaka 2022/23.
Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini Tanzania katika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Mhandisi Yusuph Shaban akizungumzia hivi karibuni alieleza kuwa sasa Wilaya ya Songwe bado barabara nyingi ziko kwenye mazingira yasiyolizisha lakini kupitia mgawanyo wa bajeti hiyo wanategemea kuwa sura ya Wilaya kiusafiri na usafirishaji itakuwa na unafuu mkubwa.
Mhandisi Shaban ameeleza kuwa kwenye bilioni hiyo bilioni 2.07, takribani bilioni 1 ambazo zinatoka kwenye tozo ya Mafuta itaenda kufungua barabara muhimu kiuchumi na zile zenye mahitaji na manufaa kwa wananchi.
Amechanganua kuwa milioni 350 zinaenda kufungua mtandao wa barabara Kapalala – Gua ambapo ni km 10, milioni 202 inaenda kufundua barabara ya Galula – Mbuyuni ni maboresho ya km 5, maboresho ya barabara ya Ifwenkenya – Ileya – Magogo kilimota 5 takribani milioni 150 itatumika na milioni 248 inakusudiwa kujenga barabara ya Mbugani – Shujila kwa umbali wa km 7.
Ameeleza kuwa milioni 645 ambazo chanzo chake ni fedha za mfuko wa barabara zinakusudiwa kwenda kuboresha barabara (matengenezo ya kawaida katika mtandao uliopo).
Pia, Mhandisi Shaban ameelza kuwa milioni 500 ambazo zinatoka mfuko wa jimbo kama ambavyo ilikubalika kwenye vikao vya Baraza la Madiwani kuwa zitaendelea kujenga barabara za mitaa kiwango cha lami km 1 ambapo kwa mwaka huu wa fedha mitaa ambayo itajengwa ni mtaa wa Kata, Ruyenga, Boma na Mwamalai.
Mchakato wa manunuzi umekamilika na wakandarasi wamepatikana na baadhi yao wapo maeneo ya kazi na wengine wanajipanga kimitambo kwa ajili ya kuanza kazi.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.