Mhe. Simon Simalenga, Mkuu wa Wilaya ya Songwe amewaongoza mamia ya wananchi na wanafunzi kupanda miti eneo la kuzunguka Shule ya Sekondari ya Namaraji iliyopo Kata ya Totowe ikiwa ni sehemu ya kuenzi Mapinduzi Matukufu ya 59 ya Zanzibar.
Mhe. Simalenga kabla ya kuanza kupanda miti akizungumza kwenye eneo hilo leo Januari 12, 2023, amewasihi wananchi kuwa na utaratibu wa kupanda mti bila kusubiri amri au kauli ya serikali kwani utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mmoja.
Amesema "Tumeona ni vyema kupanda miti siku hii (Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar) ili kuunga mkono na kuenzi yale ambayo waasisi wetu walikuwa wanafanya katika utunzaji wa mazingira", alisema Mhe. Simalenga.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songwe Mhe Godian Wangala ambaye ni diwani wa Totowe ameishukuru serikali kwa kuichagua Namaraji na kata ya Totowe kuwa sehemu ya mfano kupanda miti.
CPA. Cecilia Kavishe, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Songwe amesema Halmashauri imeshaotesha miche ya aina mbalimbali ambayo itapandwa kwenye maeneo tofauti tofauti kwa ajili ya kuendelea kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Nao baadhi ya wananchi wakizungumzia zoezi la upandaji wa miti wameipongeza serikali huku wakiahidi watakuwa mabalozi katika kuitunza miti iliyopandwa.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.