Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe CPA. Cecilia Kavishe amefanya kikao na Watendaji wa Kata kwa lengo la kuwaeleza juu ya mfumo mpya wa Serikali wa ukusanyaji mapato unaofahamika kwa jina la TAUSI.
CPA. Cecilia Kavishe amewaeleza watendaji hao kwenye kikao kilichofanyika Ukumbi wa Sambila Machi 10, 2023 kuwa mfumo huo mpya unalenga kuongeza ufanisi katika makusanyo mapato na itasaidia kupunguza usumbufu kwa wananchi na watendaji wa vijiji na kata.
Itakumbukwa kuwa kabla ya ujio wa mfumo huo, Serikali ilikuwa inatumia mfumo wa LGRCIS, au Local Government Revenue Collection Information System ambao ulishindwa kuendana na kasi ya mahitaji ya kisasa.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji huyo amewahimiza watendaji kuendelea kujipanga na msimu wa mazao upande wa stakabadhi ghala ambao kwa Wilaya ya Songwe utakuwa unafanya kazi kwa mara ya kwanza
Amesema endapo watendaji wa kata na vijiji watawajibika ipasavyo mfumo wa stakabadhi ghalani utakuwa rahisi lakini inaweza ikawa tofauti endapo kutakuwa na kutegeana katika kutimiza majukumu kwenye maeneo husika.
Pamoja na hayo, watendaji wamekumbushwa kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato hali kadhalika kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo inatekelezwa kwenye vijiji na kata husika, CPA. Kavishe amedai kuwa watendaji wa kata watapimwa uwezo wao wa kiuongozi kupitia mapato na usimamizi mzuri wa miradi ya serikali.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.