Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Simon Simalenga ametimiza usemi wa waswahili kuwa ahadi ni deni, kwani naye ameamua kulipa deni la kuahidi kuwapatia vifaa vya michezo klabu ya Saza FC iliyopo Kata ya Saza ambapo ameanza kwa kutoa mipira minne kila mmoja unathamani ya laki moja.
Mhe. Simalenga amesema Wilaya ya Songwe imebarikiwa kuwa na vipaji vingi ambavyo vimekosa msaada wa kufikishwa mbali, akisema kupitia mipira hiyo minne Saza FC watakuwa kwenye nafasi ya kushiriki kwenye mashindano mbalimbali pamoja na maandalizi ya wakati.
Akieleza sababu ya kuanza na mipira baada ya vifaa vingine, Mhe. Simalenga ameeleza kuwa ni rahisi kushiriki mpira wa miguu ukiwa na mpira hivyo aliona ni muhimu kutoa kwanza mipira badala ya vitu vingine ingawa navyo ni muhimu.
Naye kocha wa Saza FC Issa Abddalah akizungumza kwa niaba ya wachezaji wa timu hiyo mbele ya mkuu wa wilaya ameshukuru kwa kuwapatia zawadi ya mipira kwani walikuwa wanakabiliwa na uhaba wa mipira, hata hivyo amemuomba kuendelea kuiunga mkono timu hiyo kwenye maeneo mengine ya vifaa kama jezi, fulani za mazoezi na miundombinu ya uwanja.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe ameendelea kutembelea maeneo mbalimbali ambayo alitoa ahadi ya vitu mbalimbali na kwenda kulipa kama ambavyo alifanya Sume Sekondari kupeleka viti, Maweni Sekondari amepeleka pia mipira yenye thamani sawa na ile ya Saza FC.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.