Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Solomon Itunda ameomba kupandishwa kwa hadhi kwa barabara ya Kininga kwenda Ngwala yenye kilomita 48 na Kapalala - Gua ili ziwe kwenye orodha ya barabara zinazohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa lengo la kupata matengenezo na marekebisho ya mara kwa mara.
Mkuu wa Wilaya huyo ametoa maombi hayo wakati akizungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Songwe kilichofanyika Ukumbi wa Nselewa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Machi 06, 2023.
Maombi ya barabara hizo ni kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo zinafanyika kwenye maeneo yao. Kininga kwenda Ngwala ni barabara ambayo inategemewa kuwapokea wachimbaji wa madini ya rare earth kutoka kwa kampuni ya Peak Resources.
Wakati barabara ya Kapalala kwenda Gua husaidia kusafirisha mazao ya kimkakati yanayolimwa kwenye kata ya Gua likiwemo zao la Tumbaku, mahindi na baadhi ya wananchi kuanza kulima korosho.
Kufuatia maombi hayo, Bodi ya Barabara imeridhia ombi la kupandishwa hadhi kwa barabara moja ya Kininga - Ngwala ambayo sasa itakuwa inahudumiwa na TANROADS Mkoa wa Songwe.
Wilaya ya Songwe ni Wilaya ya kimkakati kutokana na kuwa na madini ambayo yamekuwa yakichangia pato kubwa kwa taifa na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.