halimashauri ya wilaya Songwe una hali nzuri ya hewa na mvua za kutosha kuwezesha kuzalisha mazao ya kilimo. halimashauri inakadiriwa kuwa na jumla ya Hekta 1, 918,776.94 zinazofaa kwa kilimo, kati ya hizo jumla ya Hekta 411,575 zinalimwa mazao ya chakula na Hekta 134,343 mazao ya biashara.
Mazao makuu ya chakula yanayozalishwa Mkoa wa Songwe ni Mahindi, Mpunga, Maharage Mtama na Karanga. Mazao mengine ni Viazi Mviringo, Viazi Vitamu, Mhogo, Njegere, Mboga na Matunda. Mazao ya Hahindi, Mpunga na Maharage pamoja na kutumika kama mazao makuu ya chakula, ziada inayopatikana huuzwa ili kuongeza kipato cha wakulima.
Mazao makuu ya biashara yanayolimwa Mkoa wa Songwe ni Kahawa, Tumbaku, Iliki, Pareto, Alizeti, Ufuta na Kiasi kidogo cha zao la Kokoa linalolimwa katika kijiji cha Kapeta kinachopakana na Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Kyela.
Mwaka 2016/2017 Hekta 411,575 zililimwa mazao ya chakula na kuvunwa tani 995,051 hadi kufikia Juni 2017, sawa na 92% ya lengo la Mwaka la tani 1,070,457. Mahitaji ya chakula katika Mkoa inakadiriwa kufikia tani 467,355, hivyo kuwa na ziada ya tani 527,696.
Mchanganuo wa utekelezaji wa malengo ya uzalishaji msimu wa 2016/2017 umeoneshwa kwenye Jedwali
Jedwali: Uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Biashara hadi Juni, 2017
Halmashauri |
Malengo ya Mazao ya Chakula |
Utekelezaji wa Mazao ya Chakula |
Malengo ya Mazao ya Biashara |
Utekelezaji wa Mazao ya Biashara |
||||
Eneo (Ha) |
Uzalishaji (Tani) |
Eneo (Ha) |
Uzalishaji (Tani) |
Eneo (Ha) |
Uzalishaji (Tani) |
Eneo (Ha) |
Uzalishaji (Tani) |
|
Ileje
|
80,110 |
384,831 |
81,210 |
489,651 |
10,396 |
6,936 |
10,204 |
6,760 |
Songwe
|
42,929.00 |
106,469.00 |
31,197.21 |
59,917.47 |
34,280.00 |
59,889.70 |
14,435.02 |
12,232.21 |
Mbozi
|
184,160 |
391,715 |
112,746 |
336,757 |
67,679 |
43,813 |
67,679 |
38,117 |
Momba
|
92,219 |
166,222 |
67,984 |
98,152 |
19,590 |
23,794 |
19,590 |
18,338 |
Tunduma TC
|
12,157.16 |
21,220 |
6,246 |
10,574 |
2,398 |
1,561 |
1,762 |
1,102 |
JUMLA
|
411,575 |
1,070,457 |
299,383 |
995,051 |
134,343 |
135,994 |
113,670 |
76,549 |
Chanzo: Halmashauri za Wilaya, na Mji wa Tunduma 2017
Jedwali: Wastani wa bei za mazao sokoni kufikia 15 Desemba, 2017
Na
|
Aina ya Chakula
|
Upatikanaji wa
Chakula Sokoni |
Bei ya chini
kwa kilo |
Bei ya juu
kwa kilo |
Wastani wa bei
Kwa kilo |
1
|
Mahindi
|
Kinapatikana
|
278
|
361
|
320
|
2
|
Mchele
|
Kinapatikana
|
1900
|
2200
|
2050
|
4
|
Ulezi
|
Kinapatikana
|
800
|
1000
|
900
|
6
|
Viazi vitamu
|
Kinapatikana
|
500
|
600
|
550
|
7
|
Maharage
|
Kinapatikana
|
1,500
|
2000
|
1750
|
8
|
Mikunde mingine
|
Kinapatikana
|
1,500
|
1,800
|
1650
|
9
|
Mtama
|
Kinapatikana
|
400
|
600
|
500
|
10
|
Soya
|
Kinapatikana
|
800
|
1000
|
900
|
11
|
Alizeti
|
Kinapatikana
|
350
|
500
|
425
|
12
|
Ngano
|
Kinapatikana
|
1,100
|
1,600
|
1,350
|
13
|
Karanga
|
Kinapatikana
|
1,500
|
2,000
|
1,750
|
14
|
Viazi mviringo
|
Kinapatikana
|
800
|
1,150
|
950
|
Chanzo: Halmashauri za Wilaya na Mji Tunduma 2017
MALENGO YA UZALISHAJI MSIMU 2017/2018.
Malengo ya Uzalishaji Mazao ya Chakula na Biashara 2017/2018.
Malengo ya halimashauri kwa msimu wa mwaka 2017/2018 ni kuzalisha tani 1,276,836 za mazao ya chakula na tani 136,650 za mazao ya biashara. Hali ya hewa msimu huu ni nzuri na mvua zilianza kunyesha wiki ya kwanza mwezi Novemba, 2017. Hali ya mazao kwa ujumla ni nzuri na wananchi wanaendelea na shughuli ya kupanda mazao ya chakula mpaka kufikia traehe 15 zaidi ya 75% ya wakulima wameshapanda na walio salia mpaka kufikia tarehe 15/01/2018 watakuwa wamekamilisha.
Mchanganuo wa malengo ya uzalishaji wa mazao umeainishwa katika Jedwali
Jedwali :Malengo ya uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Biashara msimu 2017/2018
HALMASHAURI |
Mazao ya Chakula |
Mazao ya Biashara |
||
Eneo (Ha) |
Mavuno (Tani) |
Eneo (Ha) |
Mavuno (Tani) |
|
Ileje
|
81,054 |
532,694 |
10,396 |
6,936 |
Songwe
|
46,981 |
94,309 |
34,245 |
59,856 |
Mbozi
|
186,189 |
461,254 |
67,679 |
43,813 |
Momba
|
92,486 |
171,123 |
19,590 |
23,794 |
Tunduma TC
|
12,425 |
17,457 |
2,502 |
2,251 |
JUMLA
|
419,135 |
1,276,836 |
134,412 |
136,650 |
Chanzo: Halmashauri za Wilaya na Mji Tunduma 2017
PEMBEJEO ZA KILIMO.
Mahitaji ya Pembejeo msimu 2017/2018.
halimashauri katika msimu 2017/2018 umepanga kutumia pembejeo za kilimo kwa upande wa mbolea za kupandia tani 43,625, kukuzia tani 62,953 na mbegu bora tani 5,772 ili kutekeleza malengo ya uzalishaji ya tani 1,276,836 za mazao ya chakula na tani 136,650 za mazao ya biashara.
Jedwali Na. 9 likionesha mahitaji ya pembejeo kwa kila Halmashauri.
AINA YA PEMBEJEO (TANI) |
MAHITAJI (TANI/LITA) TOKA KILA WILAYA |
|||||
|
|
|
|
|
|
|
MBOLEA YA KUPANDIA
|
ILEJE (1)
|
TUNDUMA TC (2)
|
MBOZI (3)
|
MOMBA (4)
|
SONGWE (5)
|
TANI/LTS
|
DAP
|
6,951 |
1,000 |
16,315 |
7450 |
3,734 |
35,450 |
NPK 20:10:10
|
104 |
0 |
2,022 |
0 |
0 |
2,126 |
NPK 10:18:20
|
255 |
0 |
1,100 |
2650 |
244 |
4,249 |
NPK 17:17:17
|
0 |
0 |
1,800
|
0 |
0 |
1,800 |
MINJINGU MAZAO
|
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
JUMLA NDOGO MBOLEA KUPANDIA
|
7,310 |
1,000 |
21,237 |
10100 |
3,978 |
43,625 |
MBOLEA YA KUKUZIA
|
|
|
|
|
|
|
UREA
|
6,473 |
1,950 |
19,565 |
6,445 |
3,834 |
38,267 |
CAN
|
2,313 |
1,300 |
8,109 |
6,445 |
98 |
18,265 |
SA
|
1,484 |
650 |
1,587 |
2,700 |
|
6,421 |
JUMLA NDOGO YA MBOLEA KUKUZIA
|
10,270 |
3,900 |
29,261 |
15,590 |
3,932 |
62,953 |
JUMLA KUU MBOLEA
|
17,580 |
4,900 |
50,498 |
25690 |
244 |
106,578 |
JUMLA KUU MBEGU BORA
|
1,205 |
380 |
2,640 |
471 |
1,076 |
5,772 |
Bei elekezi ya mbolea ya kupandia na kukuzia iliyotolewa na TFRA kwa Mkoa wa Songwe ni kama inavyoonesha katika jedwali Na. 10 kwa kila Wilaya.
Jedwali likionesha bei elekezi kwa Wilaya
Na
|
Halmashauri
|
Bei elekezi ya mbolea ya kupandia - DAP (TZS)
|
Bei elekezi ya mbolea ya kukuzia - Urea (TZS)
|
1
|
Ileje
|
54,179
|
41,600
|
2
|
Mbozi
|
54,014
|
41,435
|
3
|
Momba
|
54,300
|
41,721
|
4
|
Songwe
|
54,118
|
41,539
|
5
|
Tunduma
|
54,360
|
41,781
|
Wenyeviti wa kamati za Pembejeo Wilaya wameshauriwa kuhakikisha pembejeo zinawafikia wakulima kwa kila kata/kijiji iliwakulima waweze kupata huduma ya pembejeo kwa urahisi kwa kufuata bei elekezi ya Pembejeo iliyowekwa na Serikali, ikibidi Halmashauri zinunue pembejeo na kuwafikishai wakulima katika maeneo yao kama hakuna wakala eneo hilo.
USAMBAZAJI WA PEMBEJEO MSIMU 2017/2018.
Kupitia Mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja na bei elekezi ilitolewa na Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa mbolea Nchini (TFRA), bei hiyo inazingatiwa kwa kuhakikisha inamfikia mkulima ndani ya Mkoa kama ilivyo pendekezwa na TFRA. Makampuni na mawakala wa pembejeo ndani ya Mkoa wameweza kufikisha mbolea katika vituo vikubwa vya Vwawa na Mlowo ambao ni Export Traders, STACO, Yara Tanzania na Unyiha Associate ndipo mawakala wadogo hununua na kuzifikisha vijijini. Changamoto kubwa iliyopo ni malalamiko toka kwa mawakala wadogo ambao wanadai kutopata faida kutokana na gharama kuwa kubwa zinazohusisha usafirishaji. Kama inavyoonesha katika Jedwali namba 11 hapa chini:-
Jedwali makadirio ya gharama halisi za usambazaji mbolea
Kutoka
|
Kwenda
|
Gharama ya kusafirisha 50Kg Tsh
|
Bei ya jumla vwawa
|
Bei ya jumla pamoja na gharama za usafirishaji
|
Bei elekezi ya mbolea kila Wilaya
|
Faida/Hasara
|
||||
Mbozi
(Vwawa) |
DAP
|
UREA
|
DAP
|
UREA
|
DAP
|
UREA
|
DAP
|
UREA
|
||
Ileje
|
1,650
|
52,500
|
40,000
|
54,150
|
41,650
|
54,179
|
41,600
|
29
|
(50)
|
|
Momba
|
2,400
|
52,500
|
40,000
|
54,900
|
42,400
|
54,300
|
41,721
|
(600)
|
(679)
|
|
Tunduma
|
1,650
|
52,500
|
40,000
|
54,150
|
41,650
|
54,360
|
41,781
|
210
|
68
|
|
Mbozi
|
1000
|
52,500
|
40,000
|
53,500
|
41,000
|
54,014
|
41,435
|
510
|
435
|
|
Mbeya
|
Songwe
|
1500
|
52,500
|
40,000
|
54,500
|
41,500
|
54,118
|
41,539
|
(382)
|
(39)
|
Kwa mchanganuo huo hapo juu baadhi ya mawakala wadogo wameshindwa kufikisha pembejeo katika wilaya na kata kutokana na kutopata tija yeyote katika biashara hiyo ukilinganisha na gharama za uendeshaji. Mh. Waziri wa Kilimo Dr. Charles J. Tizeba alitolea ufafanuzi kuwa mbolea ya awamu ya pili itakayoingia mwezi Desemba itatoa mchanganuo wa bei ya jumla na rejereja kwa wakala mkubwa ngazi ya Mkoa na Wilaya pamoja na mgawanyo wa 12% ili mawakala wadogo waweze kufikisha pembejeo vijijini bila shida yeyote tofauti na ilivyo sasa.
KIASI CHA MBOLEA SAMBAZWA.
Kiasi cha mbolea kilicho wasilishwa ndani ya halimashauri kupitia makampuni na mawakala wakubwa pamoja na kiasi kilichokwisha sambazwa kwa wakulima tangu utaratibu huu wa uagizaji wa mbolea wa pamoja ni kama inavyo onesha katika jedwali namba 12 hapa chini:-
Jedwali namba 12 usambazaji wa mbolea na mawakala wa kati
Na
|
Jina la kampuni/ Wakala
|
Kiasi cha mbolea ingizwa Mkoani (Tani)
|
Kiasi cha Mbolea Sambazwa kwa Wakulima (Tani)
|
Asilimia ya usambazaji
|
1
|
Export Traders
|
19,200
|
17,264
|
90% |
2
|
STACO
|
629
|
577.6
|
92% |
3
|
Unyiha Associates
|
1000
|
950
|
95% |
4
|
Yara Tanzania
|
9,600
|
8,932.30
|
93% |
5
|
Mawakala wa kati
|
5,450
|
4,128.60
|
75% |
JUMLA
|
35,879
|
31,852.5
|
88% |
Mwaka 2017/2018 lengo la NFRA lilikuwa kununua tani 6,000 za mahindi kwa Nyanda za Juu Kusini, katika Mkoa wa Songwe, hadi mwisho wa msimu jumla ya tani 5,487.317 zilinunuliwa katika vituo vya Mkoa wa Songwe.
Jedwali Ununuzi wa mahindi katika msimu 2017/2018 Mkoani Songwe
Na |
Halmashauri/Kituo |
Tani |
1 |
Ileje
|
638.589 |
2 |
Mbozi
|
1,860.753 |
3 |
Momba
|
811.290 |
4 |
Songwe
|
157.270 |
5 |
Tunduma
|
2,019.415 |
Jumla |
5,487.317 |
Chanzo: Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya ya Chakula (NFRA) 2017
KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Katika Mkoa wa Songwe eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni 18,664.9 Ha, zilizoendelezwa ni 4,881 Ha na zinazomwagiliwa kwa njia ya asili ni 2,142 Ha, hivyo kufanya eneo la 7,023 Ha zinazomwagiliwa.
Katika mwaka 2017/2018 Mkoa unaendelea kutekeleza miradi ya kilimo katika Halmashauri zote kupitia DADPs, mapato ya ndani na wadau wengine wa maendeleo. Fedha ambazo zilipokelewa mwaka wa Fedha 2016/17 ni Jumla ya Tsh Milioni 730 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kupitia mpango wa kuendeleza skimu ndogo ndogo za umwagiliaji nchini (SSIDP – JICA).
Aidha, fedha hizo kiasi cha Tsh. Milioni 730 zimeweza kutekeleza miradi 3 ya umwagiliaji 1) Ileje skimu ya umwagiliaji ya Sasenga kwa kusakafia mfereji mkuu mita 777.5 na kuinua urefu wa banio cm 30 ujenzi umekamilika. 2). Mbozi skimu ya umwagiliaji Mbulu mlowo ujenzi wa Gabions na tuta urefu wa 150m kwa ajili ya kuzuia maji pamoja na kufukia korongo mita za ujazo 1,200, ujenzi umekamilika 3). Momba Skimu ya umwagiliaji Naming’ongo uchimbaji wa mfereji mkuu mita 2,560 na kusakafia urefu wa mita 800 ujenzi umekamilika.
Katika mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya Tsh. 622,500,000 zitatumika kuboresha miundombinu ya umwagiliaji katika Halmashauri zetu kupitia Mpango wa kuendeleza skimu ndogondogo Nchini (SSIDP – JICA)
Huduma za Ugani
Sekretarieti ya Mkoa wa Songwe pamoja na Halmashauri zake 5 inahitaji Maafisa Ugani 575 Ili waweze kutoa huduma bora za ugani kwa wakulima. Mkoa unajumla ya Watumishi wa Ugani 286, upungufu ni watumishi 289. Katika fani ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika. Jedwali namba 14 hapa chini linaonesha mahitaji ya watumishi katika Mkoa wa Songwe.
Jedwali Hali ya watumishi Mkoa wa Songwe
Na
|
Jina la ofisi
|
Mahitaji ya watumishi
|
Watumishi waliopo
|
Upungufu
|
|
Sekretarieti ya Mkoa
|
19 |
5 |
14 |
|
Halmashauri ya Mbozi
|
213 |
117 |
96 |
|
Halmashauri ya Momba
|
132 |
77 |
55 |
|
Halmashauri ya Ileje
|
94 |
37 |
57 |
|
H/Mji wa Tunduma
|
44 |
23 |
21 |
|
Halmashauri ya Songwe
|
73 |
27 |
46 |
|
Jumla
|
575 |
286 |
289 |
Chanzo: Halmashauri za Wilaya, na Mji wa Tunduma 2017
Ili kukabiliana na upungufu huu Mkoa kupitia Halmashauri zake unaendelea kuomba vibali vya ajira mpya kila mwaka, katika bajeti ya mwaka 2017/2018 jumla ya watumishi 157 Wanatarajiwa kuajiriwa. Aidha huduma za ugani zinatolewa kwa wakulima kwa kushirikiana na sekta binafsi/wadau wa kilimo waliopo ndani ya Mkoa wetu.
ZANA ZA KILIMO
Mkoa umepiga hatua katika matumizi ya zana za kilimo ambapo matrekta makubwa yapo 142, matrekta madogo 110, plau 125,753, mikokoteni 108,012 majembe ya kupalilia 78, rippers 42, majembe ya kupandia 18 na maksai 137,011 Hamasa na elimu ya matumizi ya zana bora za kilimo inaendelea kutolewa ili kurahisisha shuguli za kilimo na kuongeza uzalishaji wenye tija.
Matrekta
makubwa |
Matrekta
Madogo |
Plau
|
Mikokoteni
|
Majembe
kupalilia |
Rippers
|
Majembe
Kupandia |
Maksai
|
142 |
110 |
125,753 |
108,012 |
78 |
42 |
18 |
137,011 |
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.