UTAMADUNI KATIKA WILAYA YA SONGWE
MAKABILYA YANAYOPATIKANA WILAYA YA SONGWE
Wazawa wa wilaya hii kuna makabila yafuatayo
Wabungu wanaopatikana kata ya Mwambani,Mkwajuni,Saza,Mbangala,Kapalala,Udinde
Wamanda wanaopatikana Kata ya Gua, ni kabila ambalo lina asili ya kifipa ambao walikuwa wanaishi kandokando ya ya ziwa Rukwa,kipindi hicho cha nyuma ilikuwa ni raisi kuvuka ila baadaye ziwa lilikuwa kubwa.
Wasongezi wanapatikana kata ya Gua
Wakimbu wanapatikana kata ya Ngwala
Wasongwe wanopatikana bonde la mto Songwe
ASILI YA WABUNGU
Asili ya kabila la wabungu ni uwemba kutoka Zambia, shughuli yao kuu ilikuwa ni uwindaji hivyo walihama maeneo ya uwemba wakaingia Morogoro kijiji cha Ilonga usagala,wakatoka Morogoro wakaingia Kiwela Tabora baadaye wakahamia bonde la mlima Kwimba ndipo walipoitwa wabungu.Wakati wapo eneo la mlima kwimba kulikuwa kuna mto mkungu lakini baada ya kuona Ziwa Rukwa walipendezwa nalo sana hivyo wakahamia eneo la mwambani na baadaye wakaanza kusambaa.Walipofika mwambani waliwakuta wenyeji ambao ni wasangazila ila waliwafukuza kwa kupaka majani yaliyoitwa amaduha (maduha) wanatwanga wanaloweka wanapaka wanakuwa wekundu hivyo wenyeji walipowaona waliwaita waungu wakimaanisha wazungu hao, hivyo neno la wabungu likatokea. Ingawa wengine wanasema kwamba neno wabungu limetokea kwa sababu wabungu walikuwa wanakula wadudu waliokuwa wanapatikana kwenye miti
Hivyo walijulikana wawemba wakiwa Zambia walipokuwa morogoro walijulikana kama wasagala na walipofika bonde la mto kwimba walijulikana kama Wabungu
CHAKULA CHA ASILI CHA WABUNGU
Chakula cha asili cha wabungu ni ugali na samaki
POMBE YA ASILI
Pombe ya asili ya wabungu ni Chimbumu na Kangara
NGUO YA ASILI
Nguo ya asili ya wabungu inaitwa Ihanzo ambapo wanaume wanavaa Kanzu nyeusi na kofia nyeusi na wanawake wanavaa nguo nyeusi wanajifunga kiunoni na kwenye maziwa.Wabungu wanaposalimia wanapiga magoti
NGOMA YA ASILI YA WABUNGU
Ngoma ya asili ya wabungu inaitwa Makala au Indemba.Ikala ni linyama limoja likubwa.Ngoma hii huwa inapigwa hasa kipindi cha marithi au kama kuna ugeni wa mtu mkubwa.
MAENEO YA KIHISTORIA NA VIVUTIO VYA KITALII
KATA YA KAPALALA
Mlima huu huwa unatumika kwa shughuli za matambiko, maombi yao huwa ni kwa ajili ya kuomba mvua na kuepushiwa hali ya magonjwa .Mara nyingi maombi hayo hufanyika kuanzia kipindi cha mwezi wa nane hadi kumi. Mlima huu unategemewa kwa shughuli za matambikao na mikoa minne ambayo ni Mbeya,Sumbawanga,Iringa na Songwe. Katika eneo la mlima kuna pango,maji ambayo hayakauki wala hayaongezeki,vyungu ndani ya pango na wanyama wa ajabu. Katika eneo la mlima kuna lugha ambayo huwa inatumika hasa shughuli za matambiko zinapokuwa zinafanyika
Inasemekana kwamba katika mlima huu kuna dhahabu lakini hazihamishiki. Na pia wakoloni waliweka alama ya chuma juu ya mlima
KATA YA GUA
KATA YA NGWALA
KATA YA MKWAJUNI NA SAZA
Ziwa Magadi linalopatikana katika kjiji cha Tete kata ya Kan
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.