Wananchi wa Kata ya Ngwala Wilayani Songwe mkoani Songwe wanakaribia kuanza kupata huduma za afya katika Kituo cha Afya cha Ngwala kwani ujenzi wake kwa sasa umefikia asilimia zaidi ya 90.
Akizungumzia hatua ya ujenzi huo hivi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe CPA Cecilia Kavishe ameeleza kuwa adha ya wananchi kusafiri umbali wa 120 km kufuata huduma za afya makao makuu ya wilaya (Mkwajuni) sasa huduma hizo zitapatikana maeneo yao ambapo kwa sasa pamoja na umbali huo wanategemea Zahanari pekee.
Ujenzi huo ambao unatumia fedha za tozo ya mihamala simu ya shilingi milioni 500 ambazo zilitengwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unajenga majengo ya Wagonjwa wa Nje (OPD), Maabara na Kichomea Taka (milioni 250), awamu ya pili milioni 250 inajenga Jengo la Mama na Watoto, Jengo la Kufulia, na Kujenga Njia za Kupitia Wagonjwa (Walk Ways).
CPA Cecilia Kavishe ameeleza kuwa mategemeo ya serikali ni kuona wananchi wanaanza kupata huduma za afya katika Kituo cha Afya Ngwala kabla ya mwaka 2022 kumalizika.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.