• Maswali |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Songwe District Council
Songwe District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Maji
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Tehama
      • Ukagazi wa Ndani
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma Za Maji
  • Madiwani
    • orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha,Mipango na Utawala
      • Kamati ya Elimu Afya Na Maji
      • Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Kikao cha madiwani
      • Meeting With Chairman Of Council
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Utangulizi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fom ya Maombi
    • Utangulizi
    • Mpango Kazi
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Kilichoongelewa
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Wakuu Wa Idara Simamieni Miradi- Majaliwa

Imetumwa: February 15th, 2023

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Idara katika halmashauri zote nchini wasimamie kikamilifu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao na wahakikishe inakamilika kwa wakati ili itae huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

“Huduma za jamii ndizo zinazogusa maisha ya kila siku ya wananachi kama elimu, maji, nishati, afya na kilimo, hivyo halmashauri zetu lazima ziongeze nguvu katika maeneo hayo. Wakuu wa Idara tumieni muda mwingi kwenda kwenye maeneo ambayo miradi inatekelezwa badala ya kukaa ofisini tu.”

Ameyasema hayo Jumatano, Februari 15, 2023) wakati akizungumza na watumishi wa mkoa wa Songwe akiwa kwenye majumuisho ya ziara ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua miradi ya maendeleo na mafanikio ambayo Serikali ya awamu ya sita imeyapata katika kipindi cha miaka miwili.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Mji Tunduma kwa kujenga baadhi ya miradi kwa kutumia makusanyo ya ndani ukiwemo ujenzi wa madarasa 10 katika shule ya msingi Haisoja kwa gharama ya shilingi milioni 800, amewataka viongozi wa halmashauri zingine nchini kuiga mfano huo.

“Viongozi wa halmashauri muwe wabunifu na mtumie fursa mbalimbali zilizopo kwenye maeneo yenu ili ziwasaidie katika kuongeza mapato. “Shirikisheni na sekta binafsi hawa watawasaidia kuleta maendeleo, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha mwelekeo kwenye hili. Tambueni mchango wao, lengo la Serikali ni kuendelea kufanya kazi na sekta binafsi.”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewaelekeza viongozi wa wilaya, halmashari na wawakilishi wa wananchi waimarishe ushirikiano baina yao na watumishi wengine katika maeneo yao ili kuhakikisha azma ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo inafikiwa.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa Mamlaka………(RUWASA) waongeze wigo wa kufanya tafiti za maeneo ambayo maji yatapatikana sambamba na kuongeza ulinzi kwenye vyanzo vya maji ili kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa maji inatatuliwa. “Pia viongozi wa halmashauri tushirikiane kulinda vyanzo hivyo.”

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba ametumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia fedha kiasi cha Zaidi ya shilingi bilioni 200 kupelekwa mkoani humo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maedndeleo ikiwemo ya afya sh. bilioni 47, maji sh. bilioni 30. 7, elimu sh. bilioni 32.9, nishati sh. bilioni 53.4 na barabara sh. bilioni 27.5

Matangazo

  • HAYA HAPA MAJINA YA WANANCHI WALIOPATA VIWANJA ENEO LA KALOLENI NA SAZA October 03, 2022
  • TANGAZO LA KAZI YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI II SONGWE DC April 03, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI November 11, 2022
  • WANAHITAJIKA MAFUNDI UJENZI SONGWE DC December 07, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Siku ya Mazingira Duniani 2023: Utunzaji wa Mazingira Wasisitizwa Wilayani Songwe

    June 05, 2023
  • DC Songwe Ataka Taasisi Za Serikali Zihusishwe Kwenye Ujenzi wa Miundombinu

    June 02, 2023
  • Wananchi wa Kijiji cha Magamba Waishukuru Halmashauri ya Songwe kwa Kuanzisha Stakabadhi Ghalani

    May 24, 2023
  • ALAT Yaipongeza Songwe DC Kwa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisasa

    May 05, 2023
  • Ona Zote

Video

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU VIRUSI VYA CORONA
Ziada Video

Kurasa za Karibu

  • PReM
  • PlanRep System
  • FFARS System
  • STMIS system
  • Mfumo wa kuomba ajira za walimu kwa njia ya mtandao
  • Tovuti ya kuomba Ajira Serikalini

Viungio Vinavyoshabiana

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • e-Government Agency
  • Ofisi ya Rais IKULU
  • Ofisi ya Rais Utumishi
  • Tovuti kuu ya serikali ya Tanzania
  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe

Watazamaji Duniani

world map hits counter

Watazamaji Wageni

Dissertation-WritingService.com

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road

    Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe

    Mawasiliano: +255 (025) 2520301

    Simu: +255 (025) 2520301

    Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma Zetu

Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.