Mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe. Philipo Augustino Mulugo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa nchini.
Mhe. Mulugo ametoa pongezi hizo Jumanne Januari 03, akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Saza, Kata ya Saza ambapo amesema ruhusa ya Mhe Rais itawapa nafasi wananchi kutofautisha kati ya pumba na mahindi.
Amesema kutokana na kazi kubwa anayofanya Mhe Rais ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, vituo vya afya, barabara na huduma za maji anaamini wananchi watakuwa kwenye nafasi ya kuona kazi kubwa inayofanywa na serikali kulinganisha na vyama vingine vya kisiasa.
Katika hatua nyingine, Mhe Mulugo amewataka wachimbaji wa madini kuandaa utaratibu wa kuwapa mikataba wafanyakazi wao ili kuepukana na migogoro isiyokuwa na tija.
Mbunge huyo amesema migogoro mingi imekuwa ikitokea kati ya mchimbaji na mfanyakazi kwa sababu hakuna mikataba, akisema pamoja na kwamba wachimbaji wadogo wamekuwa wakilalamikiwa kuwadhurumu hela wafanyakazi lakini pia wafanyakazi waelewe kuna nyakati wachimbaji "Wanakosa".
Mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe. Mulugo amehitimisha ziara maalumu ya kufunga na kufungua mwaka 2023 katika Kata ya Saza ingawa kwenye awamu hiyo ametembelea kata ya Chang'ombe, Mbuyuni, Mkwajuni, na Gua.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.