Hafsa Pongwa, Afisa Lishe Wilaya ya Songwe amesema matumizi ya pombe kwa wazazi na walezi wa watoto kunachangia kasoro ya uzingatiaji wa afua za lishe kwa watoto wadogo.
Afisa Lishe huyo amesema hayo wakati wa kikao cha Tathmini ya Lishe Wilaya ya Songwe kilichofanyika Ukumbi wa Sambila Machi 22, 2023.
Hafsa amesema kuna vijiji amekuwa akitembelea na kukuta wanawake akiwa amelewa asubuhi, "Sasa najiuliza hivi kweli kutakuwa na uzingatiaji wa lishe hapa", alisema Hafsa ambaye ni Afisa Lishe.
Amewaambia watendaji wa kata ambao ni sehemu ya wajibu kwenda kuhakikisha kuwa matumizi ya pombe kupangiwa muda maalum pamoja na mama wa watoto wachanga/wadogo kutoenda na watoto kwenye maeneo ya kutumia vilevi.
Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Songwe Chesko Mbilinyi akiongea kwenye kikao hicho amesema inashangaza kwamba pamoja na Wilaya kuwa vizuri kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula, tunakuwa na uhaba wa chakula.
Amesema vile viashiria vya lishe kila ngazi lazima zihusike ili kwa pamoja elimu ya lishe na makundi ya chakula yatasaidia kupunguza udumavu.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.