Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe CPA Cecilia Kavishe ametoa kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kwa Wanafunzi wawili ambao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye mitihani ya Wilaya na Mkoa hasa mtihani wa Mock uliofanywa karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji CPA Kavishe ametoa fedha hizo Leo Ijumaa Novemba 12, 2021 baada ya kuwatembelea Wanafunzi wa kidato cha nne na kushiriki chakula cha mchana pamoja, ikiwa ni sehemu ya kuwahamasisha Wanafunzi hao kuelekea kwenye mtihani wa mwisho utakaoanza Jumatatu Novemba 15.
CPA Kavishe akizungumza baada ya kushiriki chakula cha pamoja amesema amefika kuwakumbusha umuhimu wa elimu ambapo amewataka Wanafunzi hao kutofuata ushauri wa baadhi ya watu wakiwemo wazazi/walezi ambao wamekuwa wakiwarubuni wafanye vibaya kwenye mitihani.
"Asitokee mtu aseme ufanye vibaya kwenye mtihani, elimu ni muhimu kuliko kitu kingine. Hata kama hakuna ajira ni bora usome kuliko kudanganyana mtaani".
Mhe. Pius Omboka, Diwani wa Kata ya Ifwenkenya akizungumza baada ya tukio hilo amesema ni tukio la kihistoria tangia alipoanza siasa kushuhudia Mkurugenzi Mtendaji akishiriki chakula cha pamoja na Wanafunzi na kutoa fedha yake ya mfukoni kwa ajili ya kuwahamasisha Wanafunzi, "Sitasahau".
Rose Mwakalindile, Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Songwe amempongeza Mkurugenzi Mtendaji CPA Kavishe kwa kujitoa kiasi hicho cha fedha pamoja na kutenga muda wake kushiriki chakula cha pamoja licha ya kuwa na ratiba ngumu.
CPA Kavishe baada ya kutoa kiasi hicho Wanafunzi hao Pili Makenzi na Idi Mandai wamegwana elfu 50,000 kwa kila mmoja.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.