Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Simon Simalenga amewataka wananchi wa Wilaya ya Songwe kuchukua tahadhari za makusudi kujikinga na magonjwa ya mlipuko ukiwepo ugonjwa wa Ebola ambao tayari umefika katika mataifa jirani.
Mhe. Simalenga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Waziri Kindamba ametoa tahadhari hiyo Jumanne Oktoba 04, wakati akizungumza na waamini wa Kanisa la Kikatoliki Wilayani Songwe na Wananchi ambao wamejitokeza kwenye Jubilei ya Miaka 50 ya Hospitali ya Mwambani iliyofanyika pembeni kidogo mwa kanisa la Katoliki Mkwajuni.
Mhe. Simalenga amesema kwa sababu Tanzania siyo kisiwa ugonjwa wa Ebola ambao bado nchini haujafika unaweza kufika endapo tahadhari za dhati hazitachukuliwa.
Mpaka sasa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini lakini mataifa jirani ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tayari kuna waathirika wa ugonjwa huo ambao husababisha na Kugusa maji maji ya mwili toka kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya Ebola, kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa Ebola na kugusa mizoga au kula wanyama pori kama vile Sokwe, Nyani, n.k.
Unaweza kujikinga na ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na kirusi cha Ebola kwa kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni mara unapomtembelea mgonjwa hospitalini au kumdumia nyumbani, epuka kugusa wanyama kama vile popo, nyani, au mizoga ya wanyama.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.