Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Simon Simalenga akiwa ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Mhe. Shaibath Kapingu na Mkurugenzi Mtendaji CPA Cecilia Kavishe amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba zoezi lililofanyika kijiji cha Iseche Kata ya Mwambani Leo Ijumaa Novemba 12, 2021 yakishuhudiwa na Wananchi wa vijiji vyote vya Kata hiyo.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya Mhe. Simalenga amewataka wahitimu hao kuchangamkia fursa za ajira ndani na nje ya Wilaya ya Songwe.
Amesema kwa sasa madarasa yanajengwa, ni fursa, Vituo vya Afya vinajengwa ni fursa, hali kadhalika miradi mengine ya Serikali itaanza kujengwa hivyo vijana lazima wawe karibu na washiriki kwenye kila fursa ambayo inajitokeza mbele yao.
Aidha, akijibu moja ya changamoto katika hafla hiyo, DC Simalenga ameahidi kutoa fedha za kushonea sare kwa wahitimu 20, wanaobakia watanoshonewa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji CPA Cecilia Kavishe amesema Halmashauri itapnga utaratibu mzuri wa kuwatumia vijana hao kwenye miradi ya maendeleo kwani wameonyesha kuwa na juhudi na ari ya kufanya kazi.
Mafunzo ya Jeshi la Akiba ni utaratibu wa nchi ambapo kila mwaka yamekuwa yakifanyika katika maeneo mbalimbali nchini, mwaka huu Wilayani Songwe takribani vijana 152 wamehitimu mafunzo hayo huku Wanawake wakiwa 12 pekee.
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.