Monday 16th, September 2024
@Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Simon Peter Simalenga anawatangazia Wananchi wote wa Wilayani hapa kuwa kesho Jumatatu Disemba 13, 2021 itakuwa siku ya kihistoria ambayo itashuhudiwa zoezi la utiwaji wa saini baina ya Serikali (Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan) na Kampuni ya Peak Resource.
Mkataba huo ni wa kuidhinisha Kampuni hiyo kuanzia uchimbaji wa madini adhimu duniani ya rare earth ambayo yanapatikana Kata ya Ngwala Tarafa ya Kwimba, Wilayani Songwe Mkoani Songwe.
Zoezi hilo litafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Convertional Center kuanzia saa tatu asubuhi Jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo itahudhuriwa na baadhi ya Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa mbalimbali wa Wizara ya madini na baadhi ya Wananchi kutoka maeneo husika (Ngwala, Itiziro, Kininga, Kapalala, Gua, Some, Udinde, Rukwa, Mbangala, Maleza na Saza).
Mkwajuni-Kimborokoto - Saza Road
Anuani ya Posta: P.o.Box 77 Mkwajuni Songwe
Mawasiliano: +255 (025) 2520301
Simu: +255 (025) 2520301
Barua Pepe: ded@songwedc.go.tz
Copyright ©2020 Songwe District Council . All rights reserved.